2025-01-09 07:21
Baada ya Yanga SC kufikia makubaliano na Coastal Union kumsajili Lameck lawi, Simba SC imefungua shauri la pingamizi la usajili huo kwenye kamati ya Sheria na Hadhi ya Wachezaji TFF ikiitaka Coastal Union ilipe fedha zote wanazowadai kwenye usajili wa awali wa Lawi
Kumbaka awali Simba walionesha nia ya kumsajili mchezaji huyo ambapo Simba walimtambulisha lakini mchezaji akaenda kufanya majaribio ulaya aliporejea nchini hakujiunga na timu ya Simba,huku Coastal union wakikanusha taarifa hiyo.