2025-03-17 09:33
#HABARI: Moto ambao chanzo chake hakijajulikana umeteketeza sehemu ya vizimba vya wafanyabiashara wa mbao katika soko la Sabasaba Manispaa ya Ilemela na kuharibu mali ikiwemo mitambo ya kuchana na kuranda mbao katika maeneo hayo.
Kaimu Kamanda wa Jeshi la zimamoto na uokoaji Mrakibu wa Jeshi, Elisa Mugisha amesema chanzo cha moto huo hakijajulikana na kwamba uchunguzi unaendelea kufanywa.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.
#Follow @radioonetanzania