2025-03-17 14:09
#HABARI: Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetangaza kuwa Jumanne, 18 Machi 2025, kitakutana na Msajili wa Vyama vya Siasa jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuwasilisha wito wao wa mageuzi ya uchaguzi. Katibu Mkuu wa chama, Mheshimiwa John Mnyika, ataongoza ujumbe huo, huku chama kikisisitiza msimamo wake wa “No Reforms, No Election.”